.

Motivational Quotes

Wednesday, 21 May 2014

Shuhuda

Mafanikio

Mahusiano

Mahusiano yakiyumba hakuna mafanikio

Usikate tamaa

Kamwe Usikate Tamaa, Endelea Kusonga Mbele

 
Maisha ni safari ya malengo yetu duniani. Na safari huanza pale unapojua kwanini unasafiri, unaenda wapi na kwa usafiri upi. Na katika safari ya malengo na ndoto zetu kuna mabonde, mawe na milima njiani. Wapo wale wanaokata tamaa kutokana na mabonde na milima ya maisha  na hupotezwa njiani na wapo wale ambao huendelea kupambana  bila kukata tamaa na watu hawa hula mema ya nchi, duniani. Maisha si kutuwama kama maji taka dimbwini kutokana na mabonde na miinuko njiani bali ni kutembea na kuendelea bila kukata tamaa.  

Mambo makubwa ya maisha yamefanywa na watu walioendelea kujaribu,kupigana hata katika mazingira ambayo hayana matumaini kwao.  Waswahili husema Kabla ya kukata tamaa katika maisha, jaribu tena.

Matukio ya harusi na Makena Entertainment

Makena Media and Entertainment Ltd inakuletea matukio ya harusi kwa picha....